Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM linakaribia kukamilisha ujenzi wa makazi ya dharura yapatayo 7,500 yatakayotumiwa na wakimbizi wanaoendelea kumiminika nchini Kenya. Hatua hiyo inaenda sambamba na makadiria yaliyowekwa hapo kabla yaliyotaka ifikapo Septemba 30 mwaka huu ujenzi huo uwe umekamilika.
Tangu kuanza kwa ujenzi huo Agosti 9 mwaka huu, zaidi ya mahema 5,808 yamekamilika na maafisa wa shirika hilo hii leo walitazamiwa kupiga hatua zaidi kwa kuweka mahema mengine kadhaa. Mahema hayo yanatazamiwa kutumiwa na wakimbizi kutoka Somalia ambao wengi wao
No comments:
Post a Comment