Web Toolbar by Wibiya

Wednesday, February 9, 2011

Maelfu wajitokeza tena Misri

Maelfu ya wananchi wa Misri wamemiminika katika mitaa ya mji mkuu Cairo, na kuelekea katika eneo la wazi la Tahrir, wakitaka serikali ya rais Hosni Mubarak kuachia madaraka.
Waandishi wa habari wanasema, haya ni maandamano makubwa zaidi kuonekana, tangu maandamano yaanze Januari 25.
Hatua hii inakuja licha ya tangazo la serikali la mipango ya kufanya mabadiliko ya utawala kwa njia ya amani.
Waandishi wa habari wa BBC wanasema, ujumbe kwa utawala ni mfupi tu - kuna uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wananchi wa ngazi zote wa Misri, na jitihada za serikali kutafuta muafaka hazitoshi.
Wael Ghonim, mkurugenzi wa huduma ya mtandao wa internet ya Google, aliyekamatwa na kuzibwa uso wake na majeshi ya usalama kwa siku 12, alipokelewa kwa shangwe wakati akiingia eneo la Tahrir.

BY SHADRACK MSUYA

No comments: